MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU WA WASABATO WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAO.
Watoto wakiwa sehemu yao chini ya uangalizi maalumu huku wazazi wao wakihudhuria mkutano mkubwa wa neno la Mungu unaondelea DMV kwa siku nne ikiwa leo Jumampili April 19, 2015 ndio hitimisho la mkutano huo.
Watoto wakiangalia vipindi vya watoto kwenye luninga.
Msimamizi wa watoto Tanya Muganda akielekeza jambo.
Tanya Muganda akiwapatia zawadi watoto
Jiji la Mwanza katika ubora wake!
Maeneo ya Bwiru, Mwanza |
Mawe hayo pichani huwekwa humo yalimo ili kuzuia mmomomonyoka wa ardhi mvua na upepo mkal! |
Tanzanian Mayunga Malimi is the winner of Airtel TRACE Music Star grand finale!
You chose Mayunga Nalimi! Tanzania's contestant seduced you and the judges Akon, Lynsha and Devyne Stephens. After a finale full of unexpected developments, Mayunga has been one of the only to keep his calm during his performances. That's probably why he fainted just after he heard final verdict!
Mayunga Malimi has quickly attracted judges' eyes with great live and acapella performances. He also took advantage of Laurna and Jitey failures in the last round of the finale to take the title back home.
He will now join Akon in the studio to work on his first single.
habari kwa hisani ya Issa Michuzi
HARAKATI ZA KUANZISHWA KWA KARIAKOO FAMILY FOUNDATION (KFF)
Mwenyekiti wa Kariakoo Family Foundation (KFF) Mohamed Bhinda akiongoza kikao cha Kamati ya Utendaji katika kuandaa rasimu ya katiba ya chama hicho kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni kama taasisi isiyo ya kiserikali kwa nia ya kukutanisha upya wadau wote waliozaliwa, walioishi na wenye asili ya Kariakoo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam. Mkutano huu umefanyika leo jioni Kinondoni Studio. Kulia kwa Bhinda ni katibu wa chama hicho Senpai Wahid
Mtunza hazina wa KFF Yahaya Sameja akielezea namna chama hicho cha jamii ya wana Kariakoo kitavyoweza kujiendesha kwa njia za ada, michango na misaada ya wafadhili katika kuendeleza wanachama, ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika shida na raha. Kushoto ni Mwenyekiti wa KFF Mohamed Bhinda na kati ni Makamu Mwenyekiti Tatu Lumelezi
Wana KFF wakipata mlo wa mchana wakati wa mapumziko
Jopo la kamati ya utendaji ya KFF baada ya mkutano wao leo
Ijue historia ya Linda
NI MENGI AMEZUNGUMUZA AMBAYO MIMI NA WEWE HATUKUYAJUA
Kesho Jumatatu katika kipindi cha huyu na yule cha mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia. Je Mume wake Mali walijuana nae wapi? na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. USIKOSE mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na kwanza production Michigan Alpha Igogo ambae alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda
Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta
Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho
Balozi wa IMETOSHA FOUNDATION Henry Mdimu atoa wito kwa vyombo vya habari na jamii!
Balozi Henry Mdimu akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi mjini Mwanza.
Henry Mdimu ametoa wito kwa vyombo vya habari na jamii nchini kulichukua suala la ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino kama lao ili kuiondoa nchi yetu katika aibu hii. Aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi ambao ni wadhamini wa habari wa ujio wa kamati ya Imetosha katika kanda ya ziwa.
|
Kutoka kushoto ni Salome Gregory, Henry Mdimu Mgaya, Issaya Mwakilasa na Zaytun Biboze. |
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Balozi Mdimu |
Imetosha
Kila
sauti inasikika.
PIGA
KELELE uunge mkono haki ya KUISHI
Ndugu waandishi wa habari, Mwakilishi wa Tanzania
Bloggers Network, mabibi na mabwana…..
Tuko hapa kuueleza Ulimwengu kupitia vyombo mbali mbali
vya habari juu ya harakati yetu ya IMETOSHA. Harakati hii hii imeanzishwa na mimi mwenyewe, Henry Mdimu,
mwanahabari mwenzenu ambaye nimeamua kwa moyo mmoja kuwa Balozi wa kujitolea wa
harakati za kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, maarufu kwa jina la Albino.
Mimi na ujumbe wangu tumekuja Mwanza kutambulisha
harakati za IMETOSHA na ikiwa sehemu ya kuandaa shughuli zitakazofanyika kanda
ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kupambana na mauaji na unyanyasaji wa watu wenye
ulemavu wa ngozi.
Mwezi ujao ujumbe wa IMETOSHA utakuja na kuweka kambi ya
kudumu Mwanza itakayozunguka kanda ya Ziwa na kutembelea nyumba kwa nyumba
zenye wahanga wa matukio ya mauaji na kutoa elimu kwa jamii kuwa mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi hayasababishi utajiri.
Pamoja na shughuli tutakazofanya tukiwa Kanda ya Ziwa
mwezi wa tano ni pamoja na maetmbezi ya hisani, kutakua na mpira kati ya Simba
na Yanga ambapo IMETOSH itavalisha wachezaji Thisrts zake ikiwa ni sehemu ya
kutangaza harakati zetu.
Pia tutakua na tamasha litakaloshirikisha wasanii
mbalimbali watakaotumbuiza nyimbo mbamimbali zitakazokua na ujumbe wa kukemea
na kupinga mauaji na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu
wakiteseka kwa muda mrefu. Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini
kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Hrakati hizi zimeanza baada ya kuona kadri muda
unavyokwenda matukio yamezidi kuongezeka na hali kuwa mbaya. Nashuhudia ndugu
zangu wakinyanyaswa, wakibezwa mtaanai na hata kudhihakiwa huku baadhi ya
wanaoshuhudia haya wakicheka tu.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na vyombo vya habari
vilimkariri Rasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania muheshimwa Jakaya Kikwete
akisema kesi mbili za mauaji ya watu wenye ulemavuwa ngozi zililipotiwa kwa
mwaka 2012 na 2013.
Taarifa hizo ziliongeza kuwa kti ya mwaka 2006 na 2015,
watuhumiwa 139 wameshikiliwa na kesi 35 zimeandikishwa. Watuhumiwa 73
waliachiwa huru na wengine 15 wamekutwa na makosa.
Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie
Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi yetu yenye sifa ya Amani duninia nzima. Hivyo
nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili
mauaji haya yakome.
Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji
wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki
ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. Salamu zangu
ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu
wa ngozi kuwa IMETOSHA.
Uchunguzi wangu wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu
ya watu wenye ulemavu wa ngozi hupelekea tatizo hili kukua na hatimaye kuuana
kw aimani za kishirikina. Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya haraki
hizi.
Mimi pamoja na mafariki zangu wanaoniunga mkono
tutakwenda Kanda ya Ziwa kutoa Elimu kabla tatizo hili halijaenea Nchi nzima.
Swali moja tujiulize kwa nini Kanda ya Ziwa? Tutatoa Elimu kwa njia ya ushauri
nasaha, pia wanamuziki sanaa
Nina mpango wa kwenda kanda ya Ziwa kuhangaika na hili
mpaka nione mwisho wake. Na ni rahisi kumaliza hili tatizo kabla halijaenea
nchi nzima. Maana Walemavu wa ngozi wako nchi nzima lakini jiulize kwa nini
Kanda ya Ziwa tu?
Mimi pamoja na rafiki zangu hawa, tunatoka kuelekea huko
kutoa elimu kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha. Pia tutakua na team ya
wanamuziki wanaoandaa nyimbo mbali mbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili
huu.
Wasanii hao ni paoma na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa
J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dami Msimamo. Tutaishi na jamii hii kwa muda tukiongea nao
kwa lugha yao kwa kutumia wakalimani kwa wsifahamu Kiswahili kuwashawishi
waamini hakuna ukweli katika Imani hizo.
Naamini nguvu ya vyombo vya Habari hivyo naomba
ushirikaiano wenu katika kuhakikisha tunatokomeza mauaji ya wenzetu ili mwisho
wa siku wanunuzi wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi wafukuzwe watakaanza
kuuliza jinsi ya kufanya mauaji haya.
Harakati za IMETOSHA rasmi zimezinduliwa rasmi tarehe
3/3/2015.
Mungu atubariki.
Ahsanteni
HENRY
MDIMU-0715000881 na 0787000880
Balozi
wa kujitolea
Harakati
za IMETOSHA
SALOME GREGORY 0717367309
Mratibu wa Habari- Harakati za IMETOSHA
Ujumbe mzito wa Imetosha watembelea kituo cha Buhangija mjini Shinyanga!
Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa
harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha
kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha
za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao
ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.
Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo. |
Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga |
Wajumbe wa Imetosha |
Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo |
Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha |
Alisema“Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba
wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula
mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa”
alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga
kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10.
Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis
alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho
kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.
Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa
ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284
wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo
chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa
kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.
Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho
Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watototo wimbo waupenda wa Clap your hands! |
Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga |
Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho |
Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali |
Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)